1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mandela miaka 90 leo Ijumaa

Kalyango Siraj18 Julai 2008

Asherehekea siku hii kijijini kwake

https://p.dw.com/p/Eehs
Mzee Madiba.Nelson Mandela.Picha: AP

Rais wa kwanza wa Afrika kusini mweusi,Nelson Mandela,anaadhimisha miaka 90 ya kuzaiwa kwake leo Ijumaa na anasherehekea siku hii kijini kwake mashariki mwa mji wa Cape Town.

Ujumbe unaompongeza kufikia siku hii umekuwa ukimiminika kutoka kila pembe ya dunia.

Nelson Mandela alizaliwa Juni 18 mwaka wa 1918 katika kijiji cha Qunu kilichoko kusini mashariki mwa Afrika Kusini.Anasema kuwa mtu kufikisha umri wa miaka 90 ni kitu kinachotia moyo.

Mandela anachukuliwa kama shujaa wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini mwake.Mandela, kama kiongozi wa chama kilichopigwa marufuku nchini mwake cha African National Congress ANC aliwekwa ndani mwaka wa 1964 na kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa kile kilichoitwa uhaini.

Mambo yalibadilika baada ya kiongozi wa wazungu wa wakati huo De Klerk kubadilisha sera na kuamua kuwa vyama vya wazalendo kama vile ANC cha Mandela, na vingine ni halali na kuliambia bunge la taifa hilo kuwa watu kadhaa waliokifungoni kwa sababu ni wanachama vya moja wa vyama hivyo wataachiliwa huru.

Mandela baada ya kutumikia miaka 27 ya kifungo chake aliachiliwa huru mwaka wa 1990.

Miaka minne baadae, yaani mwaka wa 1994 alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo.

Na hivyo kumfanya kiongozi wa kwanza wa Afrika Kusini mweusi .

Mwaka wa 1999 Mandela aliachia ngazi kama rais wa nchi hiyo na tangu mwaka huo amekuwa balozi wa heshima wa nchi yake.

Ameendesha kampeini mbalimbali dhidi ya Ukimwi na kusaidia nchi yake kupata nafasi ya kuandaa kombe la dunia la mwaka wa 2010 la mchezo wa soka.

Mwaka wa 2004 aliamua kujiondoa katika maisha ya kisiasa na kuishi maisha ya kawaida.

Na leo ijumaa akiwa anasherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake ujumbe kutoka sehemu mbalimbali unazidi kumiminika.Miongoni mwa waliotuma ujumbe ni rais wa Singapore SR Nathan,Sepp Blatter mkuu wa shirikisho la soka duniani pamoja na wengine.

Sherehe za Ijumaa ni za kimyakimya kijijini kwake,lakini hapo kesho jumamosi ndio kutafanyika sherehe kubwa ambapo mtangulizi wake F. de Klerk anatarajiwa kutoa hutuba.