1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manchester United mabingwa wa dunia

22 Desemba 2008

Manchester ni mabingwa wa dunia,Ulaya na Uingereza wakati mmoja.

https://p.dw.com/p/GLQH
Kombe la Ulaya na sasa la dunia.(Manu)Picha: picture-alliance/ dpa

Manchester United,mabingwa wa Ulaya na Uingereza,sasa ni mabingwa wa kombe la dunia la klabu bingwa kufuatia bao la Wybe Rooney katika lango la la Liga de Quito-FC Barcelona ni mabingwa wa majira ya baridi wa Spian baada ya kufungua mwanya wa pointi 10 kileleni. Katika serie A,Juventus yaongoza Ligi ya Itali kwa pointi 6.Timu za kanda ya Afrika mashariki na kati zajiwinda kwa kombe la CECAFA linaloanza Kampala,Uganda mkesha wa mwaka mpya na muogoleaji Britta Steffen, achaguliwa "mwanaspoti wakike wa mwaka wa Ujerumani" wakati Matthias Steiner,mnyanyua-vyema vizito ni mwanaspoti wa" mwaka wa kiume".

Manchester United jana iliitandika Liga de Quito ya Ecador bao 1:0 katika finali ya kombe la dunia la klabu bingwa mjini Tokyo,Japan na kufanya kile ambacho hakuna hadi sasa timu ya uingereza ilifaulu kufanya.Manchester sio tu ni mabingwa wa Uingereza na ulaya bali sasa ni pia mabingwa wa dunia.

Ilikuwa jogoo lao Wayne Rooney lililolifumania lango la Quito kuitawaza manchester mabingwa wa dunia.Baadae Rooneyx alisema,

"Imekuwa ndoto yangu ya maisha kutawazwa bingwa wa dunia." Rooney aliteuliwa ni mchezaji bora wa mashindano haya ya kombe la dunia la klabu bingwa kufuatia kutia kwake mabao 2 katika mpambano wa nusu-finali kati ya Manchester na Gamba Osaka.

Rooney akasema alijua kwamba inawezekana kutwaa vikombe vyote 3 mnamo mwaka mmoja,lakini anatoa shukurani kwa timu.

Manchester United inarudi nyumbani ikikabiliwa na kibarua cha kuzizuwia Liverpool na Chelsea kuvaa taji msimu huu.

jana bao la Robbie Keane liliipatia Liverpool pointi 1 katika changamoto yake na Arsenal.Arsenal lakini ilibidi kucheza na wachezaji 10 baada ya Mtogo Emmanuel Adebayor kutimuliwa nje ya uwanja na rifu kwa madhambi.

Arsenal iko pointi 8 nyuma ya Liverpool inayoongoza Premier League hadi kwa pointi 2 jioni hii Chelsea itapokutana na Everton.

Katioka matokeo mengine, Bolton Wanderers wameitoa Portsmouth kwa mabao 2-1 wakati Blackburn Rovers imeitandika Stoke City mabao 3-0.Fulham imetamba kwa mabao 3:0 mbele ya Middlesbrough.

Katika la Liga-Ligi ya Spian, FC Barcelona inatamba kweli na imetwazwa mabingwa wa majira haya ya maridi kabla ya likizo ya mwsaka mpya: Barcelona inaongoza usoni kwa pointi 10 baada ya kuizaba Villarreal jana mabao 2-1.Alikuwa Sedou Keita na Thierry henry waliolifumania lango la villarreal.Sevilla iliparamia jana ngazi ya Ligi hadi nafasi ya pili nyuma ya Barcelona licha ya kumudu suluhu tu ya 0:0 na Mallorca.

Mabingwa wa Spian,Real Madrid walitangaza jana kumuajiri Lassana Diarra kutoka Portsmouth,ligi ya Uingereza.Taarifa kutoka madrid inasema kwamba, Diarra amekubali mkataba hadi 2013.Real haikusema lakini imemuajiri chjipukizi huyo wa miaka 23 wa Ufaransa kwa kiasi gani.Taarifa zinadai Real imelipa dala milioni 27.83.

Ama Ligi ya Itali ikiendelea, Juventus Turin imeachwa bado nyuma pointi 6 na viongozi wa Ligi Inter milan walioichapa Atalanta mabao 3-1 katika mpambano wa mwisho mwaka huu wa serie A. Ligi ya Itali inakwenda likizo ya wiki tu kwa siku kuu za x-masi na mwaka mpya.Mabao kutoka nahodha wao Del Piero,Legrottaglie na la mbrazil Amauri yalisukuma usoni Juventus hadi pointi 36 kutoka mechi 17.Inter ina jumla ya pointi 42 kufuatia ushindi wao wa mabao 2-1 jumamosi huko Siena.Lazio Roma iliilaza Palermo bao 1-0.

Huko Afrika Mashariki na kati,timu za Taifa zinajinoa kwa changamoto ya mwaka mpya ya Kombe la Challenge-kombe la CECAFA nchini Uganda.

Zanzibar-anasema mwanamichezo wetu George Njongopa, inatumai kutamba na timu B wakati timu A "Zanzibar Heroes",inakuja wakati huo Ujerumani,kwa mara ya tatu.

Wanariadha wa mwaka wametangazwa na Ujerumani haikuhitaji muda kuchagua:Mwanaspoti "wakike wa mwaka" ametoka katika hodhi la kuogolea nae ni Britta Steffen na upande wa kiume, ameibuka Matthias Steiner-anaenyanyua vyuma vizito-(weughtlifter).Timu ya hoki ya wanaume ya Ujerumani ilichaguliwa timu bora ya mwaka .

Britta Steffen,akiwa na umri wa miaka 25 alishinda medali za dhahabu katika mita 100 na mita 50 freestyle kwenye michezo ya olimpik ya Beijing.

Alijipatia kura 3,683 akimpiku bingwa wa olimpik mwengine wa mashindano ya panga-fencing Britta Heidemann. timu ya wanaume ya hoki ilishinda medali ya dhahabu ya Olimpik huko Beijing na iliipiku ile timu ya Bundesliga-viongozi wa Ligi Hoffenheim.Hoffenheim ilitoka daraja ya pili msimu uliopita na imewapiku hata mabingwa Bayern Munich na kuvaa wao taji la nusu-msimu.

.