MANAGUA:Daniel Ortega atangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MANAGUA:Daniel Ortega atangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais

Kiongozi wa zamani wa kikomunisti nchini Nicaragua Daniel Ortega ametangazwa mshindi katika uchaguzi war ais uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Baraza la uchaguzi nchini humo limesema bwana Ortega mwenye umri wa miaka 60 amejizolea asilimia 38.07 ya kura baada ya kuhesabiwa kwa asilimia 91.48 ya kura.

Mpinzani wake mkuu anayeungwa mkono na Marekani anayefuata siasa za kihafidhina,Eduardo Montealegre amepata asilimia 29 ya kura na amekubali kushindwa.

Uchaguzi huo umetajwa kuwa ulifanyika vizuri.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com