1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamluki mkubwa wa kifaransa Bob Denard afariki dunia

14 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fn

Mamluki wa kifaransa maarufu kwa jina la Bob Denard,ambae kwa muda wa miaka 30 aliongoza mapinduzi kadhaa barani Afrika na katika visiwa vya Comoros,amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.Robert Denard,aliyeshikwa na maradhi ya sahau,alihukumiwa na korti ya rufaa ya mjini Paris mwezi July uliopita, kifungo cha miaka minne,mitatu kati ya hiyo, kifungo cha nje, na kutozwa faini ya yuro laki moja kwa kumpindua mwaka 2005 na kumtesa rais wa wakati ule wa Komoro Said Mohammed Djohar .Bob Denard anatuhumiwa kua nyuma ya njama zote za mapinduzi visiwani Komoro pamoja na kuuliwa viongozi wasiopungua wawili,Ali Saleh mwaka 1978 na Ahmad Abdallah mnamo mwaka 1989. Katika kitabu alichokipa jina „Corsaire de la Republique“ au „Jambazi la jamhuri“ Bob Denard amedai aliyoyafanya, mengi yalikua kwa masilahi, ya Ufaransa.