1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mambo yananawiri kwa Bayern Munich

19 Septemba 2011

Timu ya Ujerumani Bayern Munich imeendelea na kampeni yake ya kutafuta ushindi msimu huu kufuatia mabao mawili iliyoifunga timu ya Schalke 04

https://p.dw.com/p/12c1U
Franck Ribery wa Bayern Munich na Atsuto Uchida wa SchalkePicha: dapd

Bayern Munich imekamilisha ushindi wake wa nane katika mashindano yake yote na kuwa katika nafasi ya kwanza kwenye ligi hiyo.

Bundesliga Schalke Bayern
FC Schalke 04 dhidi ya FC Bayern MunichPicha: dapd

Nils Petersen aliyeingia kwa nafasi ya Mario Gomez ambaye alikuwa nje kutokana na maumivu, na Thomas Mueller walifunga mabao hayo mawili na kuipa Bayern pointi 15 kutoka mechi sita.

Kipa wa Bayern, Manuel Neuer, alicheza kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani.

Fussball Schalkes Torwart Manuel Neuer
Kipa Manuel NeuerPicha: picture alliance/dpa

Kwengineko furaha ilikuwa kwa timu ya Cologne baada ya Lukas Podolski kuifungia timu hiyo mabao 2 na kutoa pasi kwa MIivoje Novakovic kunako dakika 44 aliyefunga jingine huku naye Mato Jajaylo akilikamilisha la mwisho na kuiongoza Cologne kwa mabao 4-1 dhidi ya Bayer Leverkusen iliyofanikiwa kulifunga moja la kufuta machozi, kupitia Simon Rolfes, kunako dakika 70 katika mpambano huo wa timu za eneo la mto Rhine kwenye ligi hiyo ya bundesliga.

Nyota wa siku Lukas Podolski, alisema FC Cologne ipo katika kiwango cha wastani ambacho lazima ijikusanyie pointi zake. Lakini mtu hawezi kuangalia nyuma na kusema kuwa timu hiyo ipo katika njia iliyo sawa, ameongeza kuwa labda itakapocheza michezo mingine miwili na kushinda.


Ulikuwa ushindi wa kwanza wa Cologne mjini Leverklusen tangu Aprili mwaka 1996.

Fußball Bundesliga FC Köln vs. Bayer 04 Leverkusen
Picha: picture-alliance/dpa

Borussia Monchengladbach imeifunga Hamburg iliyopo chini kwenye orodha ya ligi 1-0.

Wakati huo huo ilikuwa fedheha pale kipa wa Werder Bremen, Tim Wiese alipofukuzwa uwanjani wakati timu yake ilipotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Nuremberg na Wolfsburg pia ikikabiliwa na hali sawa baada ya kipa wake kuondolewa uwanjani na timu hiyo ikafungwa 3-1 na wenyeji Hoffenheim.

Hertha Berlin kwa upande wake ilitoka sare ya 2-2 na Augsburg ikiwa zote ni timu zilizopandishwa daraja kwenye ligi hii msimu huu.

Kaiserslautern ilifanikiwa kutoka nyuma siku ya Jumamosi na kuifunga Mainz 3-1. Mlinzi wa timu hiyo, Bo Svensson amesema Kaiserslautern ambayo ni timu ya wastani kwenye bundesliga, ipo chini ya kiwango cha wastani kwa hivi sasa.

Mwandishi: Maryam, Abdalla/Afpe/Ape
Mhariri:Charo, Josephat.