1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malengo ya milenia ya maendeleo:Mtazamo wa Ujerumani

20 Septemba 2010

Viongozi wa Ulimwengu wanakutana katika Umoja wa Mataifa ili kuzijadili hatua zilizopigwa za kupambana na umasikini ifikapo mwaka 2015 ukiyazingatia malengo ya milenia.

https://p.dw.com/p/PGWP
Nembo ya kampeni dhidi ya umasikiniPicha: UN


Miundo  iliyopo  sasa  katika  nchi mbalimbali haitoshelezi  katika kufanikisha lengo la keleta mfumo thabiti  wa  utawala bora duniani.Jee  sasa  pana matumaini  gani?

Wizara  ya Ujerumani ya  maendeleo  ya  uchumi na ushirikiano iliwaalika   wataalamu mjini Berlin kujadili utawala bora  duniani kwa kuzingatia  malengo  ya  maendeleo  ya Millenia.

Mnamo  kipindi  cha miaka mitano ijayo, malengo  ya  maendeleo ya Millenia  yanapaswa kufikiwa, kama  jinsi  nchi  wanachama wa Umoja wa Mataifa   walivyokubaliana  miaka 10 iliyopita.Hatua  fulani zimeshachukua hadi  sasa katikaa   juhudi  za kuyatekelezamalengo hayo, yaani  kuupunguza umasikini duniani   kote kwa nusu, kutoa elimu ya  msingi  kwa  watoto  wote na kuondoa  ubaguzi   dhidi ya wanawake.

 Malengo hayo  yanapaswa  kutekelezwa  hadi kufikia  mwaka wa 2015.

Lakini  kadri   tunavyousogelea  mwaka  huo  ndivyo  inayvozidi kudhihirika kwamba, ili  mafanikio  katika  kuyafikia malengo  hayo ya maendeleo  ya Millenia,yanatangamana   na muundo wa utekelezaji unaofanya  kazi  kwa  ufanisi.Kinachohusika  hapa   ni matatizo ya dunia na  kwa   ajili  hiyo panahitajika majawabu  katika ngazi   ya kidunia.Dirk  Messner,mkurugenzi wa chuo cha Ujerumani cha  sera za maendeleo amesema kuwa,''Tunachojadili  sasa,ikiwa   mtu anafikiria  juu  ya  utawala  wa   dunia   au ikiwa  mtu  anafikiria masuala  ya msingi kama  vile,hali ya  hewa,  chakula  an nishati, mtu  ataweza kubaini  kwamba hapa  anakabiliana   na suala la mataifa kutegemeana.Mawazo  ya  zamani yalikuwa  juu ya  nchi   kuwa  huru kwa  kadri ilivyowezekana ili iwajibike  kwa wananchi  wake.''


Shirika lisilokuwa na makali

 Lakini  sasa  tunakabiliwa  na   mazingira   ya  kutegemeana yanayopaswa  kujengwa  katika msingi wa kisiasa.Hiyo ni changamoto iliyopo  katikaa kuufikia  utawala   wa  dunia.

Flash-Galerie WM 2010 und das Geld Entwicklungsminister Dirk Niebel Südafrika Afrika Fußball
Waziri wa maendeleo wa Ujerumani Dirk Niebel:ziarani Tanzania alikokutana na wanafunziPicha: picture alliance / dpa

Mashirika ya kimataifa yaliyopo  sasa  hayatoshi   katika  kuikabili changamoto  hiyo.Mfano ni  Umoja  wa  Mataifa   wenye wanachama 189.Umoja wa Mataifa   una   uhalali  wa  kiwango   cha juu,  lakini  panapotokea  migogoro, Shirika hilo  linakosa  uwezo   wa kupitisha  maamuzi.

Au  tuchukue  mfano wa taasisi  kama Benki  ya  Dunia  na Shirika la  Fedha  la Kimataifa,IMF. Ni kweli kwamba mashirika  hayo   yana uwezo   wa  kutekeleza maamuzi  kwa  njia  ya  ufanisi, lakini hayachukui  wajibu wa kuiwakilisha  jumuiya  ya  kimataifa.Hayo yanayahusu majopo yenye nguvu  kama    ya G7 au  G8  ya  nchi tajiri   duniani.Hata  hivyo   sasa  pana  kundi  la nchi  20.  Juu  ya jumuiya  ya  nchi  hizo   20 mkurugenzi  wa chuo  cha Ujerumani  cha sera za  maendeleo   Dirk  Messner ameeleza,''Tunayo  mapinduzi madogo  ambayo   wengi  hawakuyaona.Tumeweza kuona mabadiliko, kutoka   kwenye  uchumi  wa  dunia uliokuwa unaoendeshwa  na  nchi za G 8 kwenda  kwenye uchumi  wa dunia   unaondeshwa  na  nchi  za G  20-  yaani nchi zinazoinukia kiuchumi   na  nchi nyingine    zinazoendelea."

Mkurugenzi  huyo amesema  kuwa  huo ni  mwelekeo mzuri, kwani nchi nyingi   zinazoinukia    na  zinazoendelea,   hapo awali hazikuwa  na uwezekano  wa kushiriki  katika  michakato ya maendeleo  na ya  kisiasa katika  ngazi ya  kimataifa.Mkurugeni Messner   amaeeleza kuwa  kwa  njia  hiyo   sauti za nchi zinazoendelea  zitaweza kusikika vizuri  zaidi.

Mwandishi/ Mtulya Abdu-ZPR-Kiesel Heiner

Mpitiaji/....Mwadzaya,Thelma