1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Magari na usafirishajiAsia

Malaysia yasema itaendelea kuitafuta ndege MH370

4 Machi 2024

Malaysia imesema itaendelea na juhudi za kuitafuta ndege ya shirika la nchi hiyo iliyotoweka miaka 10 iliyopita, msimamo unaotoa faraja kwa familia za waliopoteza wapendwa wao kwenye mkasa huo ulioishangaza dunia.

https://p.dw.com/p/4d7rA
Kipande kinachodhaniwa kuwa sehemu ya bawa la ndege MH370 iliyotoweka Machi 08, 2014.
Kipande kinachodhaniwa kuwa sehemu ya bawa la ndege MH370 iliyotoweka Machi 08, 2014. Picha: Hasnoor Hussain/REUTERS

Ndege ya kampuni ya Malaysia aina ya Boeing chapa 777 yenye namba za safari MH370 ilipotea mnamo Machi 8 mwaka 2014 ikiwa safarini kutoka mjini mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur kuelekea Beijing.

Ilikuwa imewabeba abiria 227 na wafanyakazi 12. Ilitoweka kwenye rada dakika chache baada ya kuruka na tangu wakati huo juhudi zote za kuitafuta hazijafanikiwa kutambua kile kilichotokea wala chombo hicho kilikopotelea.

Kuelekea kumbukumbu ya miaka kumi Waziri wa Uchukuzi wa Malaysia, Anthony Loke, amesema serikali ya nchi hiyo bado imedhamiria kuendelea na uchunguzi na tayari wameikaribisha kampuni ya utafiti wa chini ya bahari kutoka Marekani kujadili mapendezo ya awamu mpya ya utafutaji.