MALATYA UTURUKI:Watatu wachinjwa
19 Aprili 2007Matangazo
Watu watatu wameuawa katika shambulio kwenye nyumba ya uchapishaji kusini mashariki mwa Uturuki. Watu wengine wawaili walijeruhiwa katika shambulio
lililofanywa katika mji wa Malatya. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa watu hao watatu wote walichinjwa. Mmoja wao anasemekana alikuwa mjerumani. Idara za usalama za Uturuki zimefahamisha kuwa nyumba hiyo inachapisha biblia na fasihi ya kikristo.