1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makala ya Michezo

Mohammed AbdulRahman20 Novemba 2006

Schalke yachukua uongozi wa Bundesliga ,taarifa za michezo kutoka Afrika mashariki na kati na pia mashindano ya tennis mjini Shanghai yaliomalizika kwa ushindi wa Mswisi Roger Federer.

https://p.dw.com/p/CHcw
Roger Federer anayekamata nafasi ya kwanza katika orodha ya dunia
Roger Federer anayekamata nafasi ya kwanza katika orodha ya duniaPicha: AP

Kandanda :Ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga imeingia katika michuano yake ya 13. Baada ya kuipokonya uongozi Weder Bremen wiki moja iliopita, Weder Bremen nayo imeiachia ngazi Schalke. Hayo yanafuatia kufungwa kwa Stuttgart na Bayern Munich mabao 2-1 mjini Munich na Schalke kufanikiwa kuibwaga Energie Cottbus jumlaya mabao 4-2 , wakati Bremen ilishindwa kutamba mbeleya Alemania Aachen, mchezo uliomalizika sare ya mabao 2-2 . Katika msimamo wa ligi hiyo hiyo iliomaliza siku yake ya 13, sasa Schalke inaongoza kwa pointi 26 na Bremen ikibakia nafasi ya pili kwa pointi 24. Stuttgart imeshuka hadi nafasi ya tatu ikiwa pia na pointi 24 ikitanguliwa na Bremen kwa wingi wa magoli, wakati Bayern Munich ina pointi 23 ikisimama nafasi ya nne Hertha Berlin ilioibwaga Borrusia Dortmund mabao 2-1 ikiwa imetamba ugenini na inakamata nafasi tani ikiwa na pointi 21.

Nchini Uingereza ligi kuu ya England Premier League iliingia siku yake ya 13 mwishoni mwa juma, huku Manchester United ikizidi kujiimarisha katika uongozi,ikiwatangulia mabingwa watetezi Chelsea kwa pointi 3. Manchester- ilijinyakulia pointi nyengine tatu nakufikisha jumla ya pointi 34 baada ya kuilaza Sheffield United mabao 2-1 yaliopachikwa na Wayne-Rooney.

Chelsea ikionekana kuipa onyo United, ikahakikisha inazidi kuiandama baada ya kulaza Westham United 1-0, wakati Arsenal pamoja na kuwa na mchezo mmoja wa ziada ilishindwa kuwika nyumbani na kutosheka na sare ya bao 1-1 na Middlesbrough, matokeo yalioiweka nafasi ya nne ikiwa na pointi 22 na kuondoamatumaini ya kuweza kuifikia Manchester United. Bao la Arsenal lilifungwa na Thiery Henry.Ama nafasi ya tatu mbele ya Gunners ni Portsmouth ilioibwaga Watford mabao 2-1.

Kocha wa zamani wa FC Köln ambayo sasa iko daraja la pili Christoph Daum amekubali hatimae kujiunga tena na timu hiyo. Daum mwenye umri wa miaka 53 anayepata nafuu baada ya opereshenmi ya koo alibadili uamuzi wa awali wa kuukataa wadhifa huo na kukubali mkataba wa hadi Juni 2010. Daum alikua kocha wa Cologne kati ya 1986 na 1990 na atachukua dhamana ya timu hiyo wakati wa pambano dhidi ya Duzisburg Desemba 4. Daum aligonga mno vichwa vya habari mwaka 2000 baada ya kukiri kuwa alitumia Cocaine. Hata hivyo mafanikio yake katika kandanda kama Kocha ni ya kuvutia. Aliifanikisha Stuttgart kunyakua ubingwa wa Ujerumani 1992 na ubingwa mara tatu kwa timu ya Beskitas katika ligi ya Uturuki na pia Fernebahce ilionyakua ubingwa wa nchi hiyo ikiwa chini ya Daum 2004 na 2005. Kwa hivi sasa Cologne iliowahi kunyakua ubingwa wa ligi kuu mara tatu, iko nafasi ya 10 kaika daraja la pili, na hivi karibuni ikaachana na kocha wake Mswisi Hanspeter Latour.

Mchezaji wa zamani wa kimataifa nchini Mexico HugoSanchez mwenye umri wa miaka 48 anayetajwa kuwamchezaji bora wa wakati wote nchini humo, ameteuliwakuwa Kocha wa timu ya taifa, akichukua nafasi inayoachwa na mpinzani wake mkuu Ricardo la Volpe.Sanchez aliyeshinda mataji matano ya ubingwa wa ligiakiwa na Real Madrid ya Uhispania kuanzia 1986,alishika pia taji la kuwa mfungaji magoli mengi mara tano katika ligi hiyo. Ricardo la Volpe alijiuzulu mkuwa Kocha wa Mexico baada ya Mexico kutolewa wakati wa mashindano ya kombe la dunia yaliofanyika Ujerumanina sasa amejiunga na Boca Juniors ya Argentina.

Na katika uwanja Tennis.:Mashindano ya Tennis ya mjini Shanghai Uchina yamemalizika kwa ushindi wa Mswisi Roger Federer anayeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya wachezaji bora duniani. Katika fainali ya mashiindano hayo Federer alimpa darasa Mmarekani James Blake kwa kumfunga seti 3-0, matokeo yakiwa ni pointi 6-0,6-3 na 6-4. Ni ushindi wa tatu wa taji hilo baada ya kulinyakua 2003 na 2004. Fereder alifuzu kuingia nusu fainali alimtoa hasimuyake mkuu Rafael Nidal wa Uhispania na Blake akamfunga Muargentina na bingwa wa mwaka jana wa mashindano hayo David Nalbandian. Taji hilo la Shanghai ni la 12 kwa Federer katika mashindano aliyoshiriki mwaka huu.