Mahojiano na mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
26 Septemba 2007Matangazo
Kiongozi huyo wa jeshi ametangaza kuandaliwa kwa vituo maalum vya kuwapokea waasi wanaotaka kujiunga na jeshi la taifa huku mapigano yanaendelea. Majeshi ya serikali na waasi walifikia makubaliano ya kusitisha vita mwanzoni mwa mwezi huu yaliyosimamiwa na ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini humo MONUC.
Mwandishi wetu John Kanyunyu alikuwa katika eneo la Goma na kuzungumza na kiongozi huyo wa jeshi. Anaanza na kumuuliza kwanini amewaagiza raia kurudi kwao huku waasi wakirandaranda.