1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahojiano kuhusu kifo cha afisa wa tume ya uchaguzi Kenya

John Juma
31 Julai 2017

Mwili wa meneja wa teknolojia na mawasiliano wa tume inayosimamia uchaguzi Kenya IEBC Chris Musando umepatikana, siku tatu tu baada ya afisa huyo kutoweka

https://p.dw.com/p/2hSYy

Baada ya mwili wa meneja wa teknolojia na mawasiliano wa tume inayosimamia uchaguzi Kenya IEBC Chris Musando kupatikana, siku tatu tu baada ya afisa huyo kutoweka, serikali imechukua hatua ya kuimarisha usalama wa mwenyekiti wa tume hiyo kwa kumpa askari w aziada. Mwili wa meneja huyo ulipatikana ukiwa na majeraha, katika hifadhi ya maiti jijini Nairobi. Hata hivyo tume yenyewe inasema haijaarifiwa kuhusu hilo. Mtangazaji Lillian Mtono amezungumza na makamu mwenyekiti wa IEBC, Connie Nkatha Maina anayeanza kwa kuzungumzia kifo hicho.