1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya upatanishi kuamua rufaa za wanariadha wa Urusi

Sekione Kitojo
22 Januari 2018

Mahakama ya upatanishi imeanza kusikiliza rufaa za wanariadha wa Urusi ambao walipigwa marufuku maisha kushiriki michezo ya olimpiki

https://p.dw.com/p/2rJtf
Schweiz CAS in Lausanne
Makao makuu ya mahakama ya upatanishi katika michezoPicha: picture-alliance/dpa/F. May

Mahakama  ya  upatanishi  katika  michezo  imeanza  wiki nzima ya  kusikiliza  rufaa  kwa  wanariadha  39  wa  Urusi  ambao wamefutiwa ushindi wao  katika  michezo  ya  Olimpiki  ya mwaka  2014  mjini  Sochi , Urusi kwa  kushiriki  katika  mpango wa  taifa  hilo  wa  kutumia  madawa  ya  kuongeza  nguvu  misuli , yaani  doping.

Deutschland Sport Anti Doping Polizei
Madawa ya kuongeza nguvu misuli, dopingPicha: Sean Gallup/Getty Images

Mahakama  hiyo  ya  CAS inatarajia  kutoa  hukumu wiki  ijayo. Baadhi  ya  wanariadha  wanamatumaini  ya  kubadilisha hukumu  za  kutoshiriki  mashindano  ya olimpiki maisha   na kushiriki  katika  michezo  ya  olimpiki  ya  majira  ya  baridi  mjini Pyeongchang  nchini  Korea kusini.

Mashahidi  wawili  muhimu, mtu  aliyefichua njama  za  Urusi za kutumia  madawa  hayo Grigory Rodchenkov  na mchunguzi  wa shirika  la  kupambana  na  madawa  hayo duniani  Richard McLaren , wanatarajiwa  kutoa  ushahidi kwa  njia  ya  vidio  ama kwa  simu  katika  kusikilizwa  kwa  kesi  hizo ambako kunafanyika  kwa  faragha katika  kituo  cha  mikutano mjini Geneva.

Yuliya Stepanova
Mwanariadha wa Urusi Yuliya StepanovaPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Na  rais  wa  FIFA Gianni Infantino  na  mwenzake  wa  shirika  la vyama  vya  riadha  duniani IAAF Sebastian Coe  huenda wasiwekwe  katika  uanachama  wa  kamati  ya  kimataifa  ya Olimpiki  mwezi  ujao  licha  ya  kusubiri  kwa  miaka  mitatu, duru zimesema  hii  leo.

Mashirika  hayo  mawili  ya  kimataifa , miongoni  mwa  michezo maarufu  katika  olimpiki , yamepuuzwa  tangu  mwaka 2015 wakati  wakihangaika kupambana  na  rushwa iliyotanda  katika mashirika  yao  pamoja  na  kashfa  za  rushwa ambazo zimechafua  heba  yao.

Russland FIFA Präsident Gianni Infantino - FIFA Confederations Cup Russia 2017
Rais wa FIFA Gianni InfantinoPicha: Getty Images/M. Hangst

IOC inachagua  wanachama  wapya  katika  kikao  cha  kila mwaka  ambapo  orodha  ya  majina  yaliyopendekezwa yanachapishwa  siku  chache  kabla  ya  kupigiwa  kura.

 

Mwandishi :  Sekione  Kitojo / ape / rtre / dpae

Mhariri: Iddi Ssessanga