1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini

8 Agosti 2011

Mgogoro wa fedha nchini Marekani na Ulaya na balaa la njaa nchini Somalia na katika pembe ya Afrika ndizo mada zilizohanikiza magazetini hii leo.

https://p.dw.com/p/12Ctp
Maandamano dhidi ya mgogoro wa bajeti mjini Washington

Tuanze lakini na mgogoro wa fedha unaozitikisa nchi za Ulaya na Marekani.Gazeti la "Leipziger Volkszeitung" linaandika

Ni funzo la kutisha la kashehe inayozikumba nchi za magharibi-Ni sawa na janga la moto linaloenea katika sehemu iliyosalia ya dunia.Madhara yake kwa imani ya walimwengu kuelekea masoko ya hisa na nguvu za kisiasa na kiuchumi za ulimwengu wa magharibi ni makubwa kupita kiasi.Kwamba hivi sasa China- nchi ya kiimla,inayofuata mfumo wa kikoministi ndio inayoipa funzo Washington,hali hiyo inaifanya Marekani inayoongozwa na Obama idhalilike.Balaa la madeni sio tu litadhuru hali ya kujiamini ya Marekani ,litakuwa na madhara mfano wa yale yaliyotokea ilipolazimika kuwarejesha nyumbani wanajeshi wake toka Vietnam au wakati wa mashambulio ya kigaidi ya wafuasi wa itikladi kali ya dini ya kiislam dhidi ya minara miwili ya mjini New-York-september mwaka 2001.

Gazeti la "Mannheimer Morgen" linaonya na kuandika:

Börsen reagieren
Masoko ya hisaPicha: picture alliance/dpa

Hali inayojitokeza kuwa tulivu humu nchini ni ya hadaa,kwasababu migogoro ya fedha inayozikaba nchi mfano wa Marekani,Italy,na Hispania inadhuru pia biashara ya nje ya Ujerumani.Si bure kwa hivyo kuiona China ikikosoa uzembe wa kisiasa wa Marekani kwa kushindwa kukubaliana juu ya namna ya kuufumbua mgogoro wa fedha.China sio tu inahofia kuona mali yake ikipungua thamani bali pia inahofia kupoiteza mteja wake mkubwa kwa bidhaa zake zisizokuwa na thamani.

Mada yetu ya pili magazetini inahusu balaa la njaa nchini Somalia na katika pembe ya Afrika kwa jumla.Gazeti la "Delmenhorster Kreisblatt" linaandika:

Walimwengu wanafumba macho moja kwa moja majanga ya vita na njaa yanapopiga barani Afrika.Na hali hiyo hasa ndiyo inayowavutia waimla na wanamgambo.Na hali hiyo hasa ndiyo inayobidi kubadilika.Afrika inahitaji ushirikiano wa kudumu na wa kutegemewa ili iweze kuimarisha miundo mbinu yake ya kidemokrasia na kujikinga dhidi ya majanga ya ukame.Jumuia ya kimataifa ikifanikiwa kufanya hivyo,basi pengine janga jengine la njaa litaweza kuepukwa.

Gazeti la Schwäbische Zeitung linahisi:

Somalia Hungersnot Lager Flüchtlingslager Kind
Balaa la njaa nchini SomaliaPicha: dapd

Hili si janga la kimaumbile linalowaathiri watu zaidi ya milioni 10 katika pembe ya Afrika.Janga hili limesababishwa na binaadam.Mabadiliko ya tabia nchi,idadi kubwa ya wakaazi na sera za kilimo za dunia zinazozingatia masilahi ya Marekani na Umoja wa ulaya zinawazuwia waafrika mashariki kuweza kujiendeleza.Nchini Somalia vita ndivyo vinavyochangia kwa sehemu kubasa.Hata hivyo mtu anashindwa kuelewa kwanini watu wanakufa kwa njaa katika maeneo ya kaskazini ya nchi ambazo takriban ni tulivu,yaani Kenya,Uganda na Ethiopia.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed