Magazeti ya Ujerumani hii leo yameandika kuhusu ziara ya waziri mkuu wa Israel nchini humo. | Magazetini | DW | 13.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Magazeti ya Ujerumani hii leo yameandika kuhusu ziara ya waziri mkuu wa Israel nchini humo.

Ziara ya waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert nchini Ujerumani na ishara aliyoitoa kuwa nchi yake inamiliki silaha za kinuklia, ni mada ambayo imewashughulisha wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo Jumatano. Moja ya masuala magumu yaliyopo ni jinsi ya kuutetea msimamo wa Israel. Katika udondozi wa magazeti ya Ujerumani hii leo huyu hapa Sekione Kitojo.

Mhariri wa gazeti la Ostsee-Zeitung kutoka Rostock anaandika kuwa hivi sasa waziri mkuu huyo wa Israel anataka kupigiwa kifua na Ujerumani. Mhariri anasema , Olmert amekwisha pata anachotaka. Lakini pamoja na hayo hajatumia busara sana. Kwanza alikosoa sana isivyokawaida ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani nchini Syria, baada ya hapo pia uhusiano wa kibiashara kati ya Ujerumani na Iran.Hofu ya Israel dhidi ya silaha za kinuklia za Iran inaeleweka. Matamshi hayo ya Olmert hata hivyo hayakuwa ya kidiplomasia na hayakustahili.

Mhariri anasema kuwa uhakika wa Israel kuwapo ni msingi wa sera za mambo ya kigeni za Ujerumani. Na katika hilo kansela Angela Merkel hakuwa na wasui wasi nalo.

Mhariri wa gazeti la tagesspiegel la mjini Berlin, anaandika kuwa George W. Bush na Ehud Olmert wakisisitiza msimamo wao wa kutokuzungumza na wale wanaowaona maadui kwa gharama yoyote ile ni kinyume na utaratibu. James Barker na Tony Blair wanaokubali moja kwa moja kuwa suala la kuzungumza na mataifa yale yanayoonekana kuwa ni adui pia nao wanaonekana kuwa mazuzu. Serikali ya Ujerumani inaweza kuwa imegundua wazo la kati kwa kati. Kauli mbiu inasema : Tunaweka mbinyo mkali dhidi ya Iran, lakini tunaonyesha aina fulani ya mnyumbuliko kuielekea Syria. Tunaitenga Iran, lakini tunatafuta mahusiano ya karibu na Damascus.

Tofauti hii inawiana na mtazamo rasmi wa serikali ya Marekani.

Nae mhariri wa gazeti linalochapishwa Neubrandenburg, la Der Nordkurier linaandika kuwa , Kansela Angela Merkel amemweleza mgeni wake waziri mkuu wa Israel kuwa mazungumzo ya kundi la pande nne kuhusu mashariki ya kati kukiwa na juhudi za Ujerumani ni lazima yaendelezwe. Huo ni ujumbe muhimu, hata kama kuna nafasi ndogo uliowekwa kwa jamii. Na matamshi ya Olmert ambayo si ya kawaida za juhudi za kuwa na mazungumzo na Wapalestina yana mwelekeo mwingine kuliko ilivyokuwa hapo zamani.

Gazeti la Frankfurter Allgemeinen Zeitung linasema kuwa , Israel haitaki kufanyika kwa mkutano wa mashariki ya kati ambao hauko katika udhibiti wake, kwani ikiweza kupata muafaka , itagharamika. Na mazungumzo ya kufikia lengo hilo na wapalestina lisihusishe kwa sasa utawala wa sasa wa chama cha Hamas. Kwa msimamo huu wa Olmert kwa mara nyingine tena ameonyesha kuwa , Israel inaweza kijeshi kuchukua hatua.

Tukibadilisha mada , kuungama kwa waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert , kuwa nchi yake ina silaha za kinuklia, gazeti la Allgemeine Zeitung kutoka Mainz, linachunguza kuwa , hakuna mwanasiasa wa Israel aliyekanusha wasi wasi huu, na kwamba suala la silaha za kinuklia la nchi hiyo haliwezi kujadiliwa, ama ama viongozi kukiri kuwa zipo. Linabaki kuwa swali , iwapo Ehud Olmert ameropoka tu ama alikuwa analizungumzia suala hili kwa ukamilifu. Hakuna cha kukana kwa mujibu wa mafanikio ya kisiasa aliyoyapata hapo zamani, na sasa kuwa na hofu kwamba hakujua alichokuwa akikizungumzia. Kukiri huko badala yake kunaashiria kukosolewa kukubwa ndani ya Israel wakati atakaporejea.