1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu wangali wakingojea misaada Bangladesh

19 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJKz

Helikopta zinapeleka chakula na dawa kwa mamia elfu ya watu walionusurika na kimbunga kilichopiga nchini Bangladesh.Kwa mujibu wa serikali,hadi watu 3,100 wamepoteza maisha yao na idadi hiyo huenda ikafikia 10,000.Sasa kuna hofu kuwa maiti za binadamu na mifugo zinazoelea majini huenda zikaeneza magonjwa.

Kimbunga Sidr kilichovuma Alkhamisi iliyopita,kwa mwendo wa kilomita 250 kwa saa kimeteketeza vijiji vizima.Siku nne kufuatia kimbunga hicho, waokozi wangali wakijaribu kufika sehemu za ndani.Njia pekee ya usafiri ni kwa helikopta au booti.Umoja wa Ulaya na Marekani zimeahidi kutoa msaada wa zaidi Euro milioni 4 kwa kama familia 900,000 zilizokumbwa na maafa.