1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelf wakimbia makazi yao kutokana na ghasia za uchaguzi Kenya

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjJJ

NAIROBI.

Mamia kwa maelefu ya wakenya wamekimbia makazi yao ili kuepuka ghasia za kikabila zilizozuka baada ya uchaguzi wa utatanishi uliofanyika mwishoni mwa juma.

Uchaguzi huo umemrejesha madarakani rais Mwai Kibaki.Idadi ya waliokufa kutokana na ghasia hizo za siku nne imefikia watu 250. Katika tukio moja baya zaidi, watu wasiopungua 30 walichomwa hadi kufa wakiwa ndani ya kanisa moja katika eneo la Eldoret.Watu wapatao 100 walikuwa wamekimbilia mahali hapo wakitorika ghasia.Kibaki na mpinzani wake wa kisiasa,Raila Odinga wanalaumiana kwa kuwa chanzo cha ghasia hizo.Odinga anasema matokeo yaliganngwa.Mkuu wa tume ya uchaguzi ya Kenya-Samuel Kivuitu asema hajafanya makosa yoyote kwani alitangaza yale aliokuwa akipata kutoka mikoani.

Wachunguzi wa kimataifa nao wamesema uchaguzi haukufikia kiwango cha kimataifa.

Wito umetolewa kutoka Marekani,Uingereza,Umoja wa Afrika pamoja na Umoja wa Ulaya wa kukomeshwa kwa ghasia.Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika-John Kufuor anajaribu kupatanisha pande mbili husika ili kukomesha ghasia.