1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid.Wahamiaji haramu warejeshwa.

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzu

Hispania imewarejesha makwao wahamiaji 750 kutoka bara la Afrika, ambao hawakuandikishwa katika muda wa wiki moja iliyopita.

Kiasi cha wahamiaji 600 miongoni mwa hao wamepelekwa Senegal mwishoni mwa juma.

Waliobaki walirejeshwa mapema nchini Morocco, Mauritania na Guinea – Bissau.

Waziri wa mambo ya ndani Alfredo Perez Rubalcaba amesema kuwa Hispania inataka kutoa fundisho kwa wahalifu wanaofanya biashara ya kuwasafirisha watu.

Maafisa wanasema kuwa zaidi ya wahamiaji haramu 30,000 wamewasili katika visiwa vya Canary mwaka jana.