MADRID:Hispania yafukuza wahamiaji wa kiafrika
21 Mei 2007Matangazo
MADRID
Serikali ya Uhispania imewarejesha kwao zaidi ya wahamiaji 750 wa kiafrika wakiwemo watoto 30.
Wizara ya Ndani ya Uhispania imesema kuwa wengi wao ni kutoka Senegal ambao walikamatwa wiki iliyopita wakati walipokuwa wakijaribu kuingia katika kisiwa cha Canary.
Serikali ya Hispania imesema kuwa wahamiaji wote haramu watarejeshwa kwao.