MADRID: Wahamiaji wameokolewa mwambao wa Hispania | Habari za Ulimwengu | DW | 06.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MADRID: Wahamiaji wameokolewa mwambao wa Hispania

Kwa mujibu wa kundi la wahamiaji waliokolewa na meli ya mizigo ya Afrika ya Kusini nje ya mwambao wa Visiwa vya Kanary vya Hispania,wasafiri wenzao wapatao 20 walizama,baada ya boti waliokuwa wakisafiria kupasuka baharini.Wahamiaji walionusurika ni miongoni mwa kama Waafrika 25,000 waliofika visiwa vya Hispania katika juhudi ya kukimbia umasikini na kuingia Ulaya. Polisi wamesema,walionusurika ni watu wazima 7 na watoto 4.Kwa wakati huo huo mjini Luxembourg, mawaziri wa sheria na wa mambo ya ndani wa nchi za Umoja wa Ulaya,wanajadiliana njia za kuzuia mtiririko wa wahamiaji kutoka magharibi mwa Afrika.Hispania inataka msaada zaidi wa pesa kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya walinzi wanaopiga doria katika mwambao wa nchi hiyo.Mawaziri hao wa Ulaya vile vile wanachunguza upya hatua za kuanzisha sera moja ya uhamiaji ifikapo 2010.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com