1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yazuka mjini Mombasa baada ya sala ya Ijumaa

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CuOM

Polisi nchini Kenya wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya mamia kadhaa ya waandamanaji wa kiislamu wanaopinga ushindi wa rais Mwai Kibaki katika uchaguzi wa Disemba 27 mwaka uliopita.

Maandamanao ya leo yamefanyika baada ya sala ya Ijumaa katika msikiti mkuu mjini humo katika siku ya tatu na ya mwisho ya maandamano yaliyoitishwa na upinzani lakini yakapigwa marufuku na polisi.