1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yanaripotiwa mjini Mogadischu

6 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcu

Mogadischu:

Maandamano dhidi ya vikosi vya Ethiopia yamegubikwa na machafuko katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.Mamia ya wasomali wametia moto mipira ya magari na kuwavurumishia mawe wanajeshi wa serikali kulalamika dhidi ya kuingilia kati wanajeshi wa Ethiopia waliowatimua wanaharakati wa korti za kiislam.Kabla ya hapo Umoja wa mataifa ulielezea azma ya kuwarejesha watumishi wake nchini Somalia.Msimamizi wa shughuli za kusambaza misaada za Umoja ya mataifa, Margareta WAHLSTRÖM amesema hata hivyo watumishi hao waterejeshwa tuu ikiwa usalama wao hautakua hatarini na wakipatiwa hakikisho la kuwahudumia wale wanaohitaji kusaidiwa.Marekani na Umoja wa Ulaya wameelezea utayarifu wa kugharimia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika nchini Somalia..Uganda imesema iko tayari kuchangia wanajeshi.Wakati huo huo mpango wa kuwapokonya silaha kwa nguvu wasomali umeakhirishwa kwa muda usiojulikana mwisho