1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabomu yaripuka Kandahar

6 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClz

Mlipuaji wa kujitolea muhanga amejilipua nje ya afisi za usalama za Marekani kusini mwa Afghanistan na kusababisha vifo vya watu wanane.Kulingana na wizara ya mambo ya ndani mlipuko huo ulikuwa mkubwa zaidi kutokea katika mashambulio yanayolaumiwa kutekelezwa na wapiganaji wa Taleban.

Wakati huohuo wanajeshi wawili wa Canada na raia wanne wa Afghanistan wamejeruhiwa katika mlipuko wa bomu la kutegwa garini mjini Kandahar hapo jana.Ghasia nchini Afghanistan zimesababisha vifo vya zaidi ya watu alfu 3 mwaka huu pekee idadi zinazoaminika kuwa mara nne ya zile za mwaka jana kwa mujibu wa ripoti rasmi.