Mabishano yanaendelea kama Zanzibar ni nchi?
18 Julai 2008Matangazo
Bado mabishano yanaendelea huko Tanzania kama Visiwa vya Zanzibar ni nchi ama sivyo. Spika wa Baraza la wawakilishi huko Zanzibar amezuwia kusikilizwa hoja ya kiongozi wa upinzani wa Chama cha CUF, Aboubakar Khamis Bakari, kutaka suala hilo lijadiliwe barazani. Spika anahoji kwamba suala hilo linajadiliwa baina ya wanasheria wa serekali za Muungano na ile ya Zazibar. Itakumbukwa kwamba chimbuko la mabishano haya lilianza pale waziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, aliposema bungeni kwamba Zanzibar sio nchi. Mwandishi wetu wa Zanzibar, Salma Said, amefanya mahojiano na Aboubakar Khamis Bakari, na alikuwa na haya ya kusema kuhusu hoja aliotaka kuiwasilisha...