Maandamano yapangwa mjini Mombasa kulaani mauaji ya Sheikh Rogo | Matukio ya Afrika | DW | 31.08.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Maandamano yapangwa mjini Mombasa kulaani mauaji ya Sheikh Rogo

Hali ni tete mjini Mombasa baada ya baadhi ya vijana wa kiislamu hii leo kupanga kufanya maandamano makubwa baada ya sala ya Ijumaa kulaani mauaji ya kiongozi wa kidini Sheikh Aboud Rogo Mohammed.

Polisi alinda gari alilokuwemo Sheikh Aboud Rogo Mohammed

Polisi alinda gari alilokuwemo Sheikh Aboud Rogo Mohammed

Hali ni tete mjini Mombasa baada ya baadhi ya vijana wa kiislamu hii leo kupanga kufanya maandamano makubwa baada ya sala ya Ijumaa kulaani mauaji ya kiongozi wa kidini sheikh Aboud Rogo Mohammed.

Sheikh Rogo ambaye anadaiwa kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la Al Shabaab, aliuwawa siku ya jumatatu na watu wasiojulikana mjini humo alipokuwa ndani ya gari lake. Awali kumekuwa na miito mbali mbali kutoka kwa viongozi wa kidini pamoja na kisiasa, kuhimiza amani baada ya ghasia za hapa na pale kukumba mji huo tangu kuuwawa kwa sheikh Rogo. Hata hivyo polisi nchini humo imesema imejitayarisha vilivyo kupambana na wale wote watakaojaribu kuyumbisha amani mjini humo.

Mwenzangu Amina amezungumza na mwandishi wetu wa mjini Mombasa Eric Ponda na kwanza anaelezea hali halisi ilivyo mjini humo.

Insert

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada