Maandamano ya kupinga vita vya Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 18.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Maandamano ya kupinga vita vya Irak

Tokyo:

Zaidi ya watu elfu mbili wameandamana katika mji mkuu wa Japan hii leo kupinga vita vya Irak.Katika kumbukumbu za kuadhimisha miaka minne tangu vikosi vya nchi shirika vinavyoongozwa na Marekani kuivamia Irak,waandamanaji hao wamedai wanajeshi wa Japan warejee nyumbani.Japan imetuma wanajeshi mia kadhaa kuwasaidia wanajeshi wa Marekani nchini Irak.Maandamano kama hayo yamefanyika jana mijini Washington,Los Angeles -Marekani na katika mihji kadhaa ya Ulaya ambako maelfu ya wapinzani wa vita waliteremka majiani.Hii leo maandamano makubwa yatakayofuatiwa na mhadhara yatafanyika mjini New-York.March 20 ijayo,itakamilika miaka minne tangu vikosi vya nchi shirika vikioongozwa na Marekani,kuivamia Irak.Wakati huo huo uongozi wa kijeshi wa Marekani umesema wanajeshi wake sita wameuwawa jana nchini Irak-wanne wameuwawa bomu liliporipuka mjini Baghdad ,mmoja katika shambulio kaskazini mashariki ya mji mkuu na wa sita ameuwawa kwa ajali mjini Tikrit.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com