1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano makubwa kufanyika leo Misri

Josephat Nyiro Charo28 Juni 2013

Vyama vya kiislamu nchini Misri vinatarajiwa kuanza maandamano makubwa leo (28.06.2013) kumuunga mkono Rais Mohammed Morsi siku mbili kabla kufanyika maandamano yaliyopangwa na upinzani.

https://p.dw.com/p/18xwz
CAIRO, June 21, 2013 (Xinhua) -- Supporters of Egyptian President Mohamed Morsi chant slogans during a protest in Cairo's Nasr City, Egypt, on June 21, 2013. Thousands of Egyptian Islamists flocked Friday to Rabaa al-Adawweya Square in Cairo's Nasr City for a rally in support of President Mohamed Morsi. (Xinhua/Amru Salahuddien) (lr) XINHUA /LANDOV
Ägypten Demonstration Mursi AnhängerPicha: picture alliance / landov

Muungano wa vyama vya kisiasa vya kiislamu na makundi kadhaa yameitisha maandamano hayo nje ya msikiti wa Rabaa al Afawiya katika mji mkuu Cairo chini ya kauli mbiu kuwa uhalali ni msitari mwekundu. Uhalali wa Rais Morsi madarakani umezua maandamano ya kumpinga na kumuunga mkono.

Wafuasi wake wanasema uongozi wake unatokana na mamlaka aliyoyapata kwa kuchaguliwa katika uchaguzi wa kwanza huru wa Urais katika historia ya nchi hiyo na kwamba changamoto anazokabiliwa nazo kama ufisadi, taasisi zilizo dhoofu, mizozo ya kiuchumi na msukosuko wa kidini ni matatizo aliyoyarithi kutoka utawala uliopita. Lakini wakosoaji wake wanamuona kama mjumbe wa udugu wa kiisalamu madarakani akiwapendelea waislamu wenye itikadi kali katika nyadhifa kuu serikalini na kulirejesha taifa hilo katika utawala wa kiimla.

Wiki iliyopita maelfu ya watu nchini humo walijitokeza kumuunga mkono Morsi wakilitaja jina lake na sheria za kiislamu na kusema kujitokeza huko kwa maelfu yao ni dhihirisho tosha kuwa ana uungwaji mkubwa nchini humo. Waislamu hao wanaushutumu upande wa upinzani nchini humo kwa kuwa mabaki ya utawala wa Rais aliyeng'olewa madarakani Hosni Mubarak wanaojaribu kupanda mbegu ya machafuko nchini humo.

Shutuma hizo zilirejelewa na Rais huyo wa Misri Jumatano wiki hii katika hotuba kwa taifa kupitia televisheni na kuonya kuwa mkwamo wa kisiasa unatishia kuilemaza Misri. Hata hivyo aliahidi kushughulikia marekebisho ya katiba na pia kufikia upinzani kwa mara nyingine tena kwa ajili ya mazungumzo. Hilo lilikuwa jaribio lake la hivi punde kujaribu kuzileta pande zote za kisiasa katika meza ya mazungumzo katika nchi ambayo imegawanyika vibaya kati ya washirika wake wa udugu wa kiislamu wenye itikadi kali na upinzani ulio na vyama vya mrego wa shoto, waliberali, wakristo na waislamu.

Bildnummer: 59152398 Datum: 30.01.2013 Copyright: imago/Sven Simon Präsident Mohammed MURSI Pressegespräch beim Staatsbesuch des ägyptischen Präsidenten im Bundeskanzleramt in Berlin, Deutschland am 30.01.2013. People Politik x0x xsk 2013 quer aktuellPolitik 59152398 Date 30 01 2013 Copyright Imago Sven Simon President Mohammed Mursi Press interview the State Visit the Egyptian President in Federal Chancellery in Berlin Germany at 30 01 2013 Celebrities politics x0x xSK 2013 horizontal aktuellPolitik
Rais wa Misri, Mohammed MursiPicha: Imago

Upinzani wapinga mazungumzo

Hapo jana muungano wa vyama vya upinzani ulipuuzilia mbali pendekezo hilo la mazungumzo na badala yake kutaka kuitishwa uchaguzi wa mapema wa Urais. Tangu kuingia madarakani mwaka mmoja uliopita, Morsi amekuwa akikabiliana na idara ya mahakama, vyombo vya habari, polisi na hata wasanii nchini humo.

Hata hivyo amekiri kufanya makosa na ameahidi kuyarekebisha. Rais Morsi amesema amefanya makosa mengi bila shaka na makosa hufanyika lakini pia yanapaswa kurekebishwa. Lakini amevionya vyombo vya habari dhidi ya kutumia vibaya uhuru walioupata uliotokana na wimbi la mageuzi la mwaka 2011.

Jeshi la Misri ambalo lina nguvu nyingi na ambalo limekuwa pembeni tangu kuchaguliwa kwa Morsi limeonya kuwa litaingilia kati iwapo kutazuka ghasia nchini humo.Maafisa wa usalama wamesema usalama umeimarishwa katika miji mikuu kujiandaa kwa uwezekano wa ghasia.

Mjini Cairo wakaazi wanatoa hela kutoka mabenki na kununua chakula cha akiba na makampuni mengi yamesema yatafunga siku ya Jumapili. Upungufu wa mafuta ya petroli umesababisha milolongo mirefu ya magari kushuhudiwa katika vituo vya mafuta na kukwamisha shughuli nyingini mjini humo na kuongeza hali ya taharuki.

Mwandishi: Caro Robi/afp

Mhariri: Josephat Charo