1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano dhidi ya sera za uhamiaji nchini Ufaransa

Hamidou, Oumilkher6 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dcst

Paris.

Maelfu ya watu wameandamana nchini Ufransa kupinga sera za uhamiaji za serikali ya waziri mkuu Francois Fillon.Kwa mujibu wa mashirika yaliyoitisha maandamano hayo,watu 20 elfu walishiriki katika maandamano hayo mjini Paris.Polisi inasema walaioshiriki ni watu 4200 tuu.Maandamano kama hayo yamefanyika pia mijini Lyon,Marseille,Toulouse na katika miji mengine ya Ufaransa.Maandamano hayo yamefanyika huku kukiwa na ripoti za kujitupa mtoni na kufa kijana mmoja wa miaka 29 wa kutoka Mali aliyetaka kukwepa asihojiwe na polisiWaaandamanaji wanaitaka serikali iwapatie wageni wanaofanya kazi nchini humo vibali vya kuishi Ufaransa.