Maafisa wa zamani wa radha kukata rufaa
2 Februari 2016Matangazo
Maafisa hao ni Papa Massata Diack, ambaye ni mtoto wa rais wa zmani wa shirikisho la riadha duniani - IAAF Lamine Diack, Mrusi Valentin Balakh-nichev na Alexei Melnikov.
Maafisa hao walishtakiwa mnamo mwezi Desemba mwaka jana kwa kosa la ukiukaji wa sheria za kupambana na dawa za kuongeza misuli nguvu.
Diack na Balakhnichev, rais wa zamani wa shirikisho la riadha la Urusi na mweka hazina wa IAAF, walipigwa faini ya pauni 17,000 wakati kocha wa Urusi Melnikov alipigwa faini ya pauni 10,000.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Iddi Sessanga