1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ma Ying-jeou ashinda uchaguzi Taiwan

22 Machi 2008

Kiongozi wa upinzani ashinda uchaguizi wa rais Taiwan

https://p.dw.com/p/DSqq
Ma Ying-jaeo pichani rais mpya wa TaiwanPicha: AP

TAIPEI

Chama kikuu cha upinzani nchini Taiwan cha Nationalist kimeshinda uchaguzi wa rais kwa vishindo leo hii na kuashiria kuboreshwa kwa uhusiano na taifa kubwa jirani yake la China ambalo linadai kisiwa hicho kinachojitawla wenyewe ni chake.

Mgombea wa chama hicho cha Nationalist au kwa jina jengine Kuomintang Ma Ying - jeou ameshinda kwa asilimia 58 ya kura wakati mgombea wa chama tawala cha Maendeleo ya Demokrasia Frank Hsieh amepata asilimia 42 ya kura.

Ma amewaambia umati mkubwa uliokuwa ukishangilia ushindi wake mjini Taipei kwamba wananchi wa Taiwan wanatarajia kuwa na serikali ilio safi isiokuwa na rushwa na kwamba watu wa Taiwan wanatarajia kuimarika kwa uchumi na kwa kuwepo kwa amani katika eneo hilo zima na hawataki vita.

Kampeni za uchaguzi huo zilikuwa zimedhibitiwa na wasi wasi juu ya kuzorota kwa uchumi na msimamo wa malumbano wa chama tawala kwa China.

Katika kampeni za uchaguzi huo Ma amekuwa akisisitiza juu ya msimamo wake kwa uhusiano na China.

Ma anasema daima wamekuwa wakishikilia msimamo wao kwamba China ni tishio kwao halikadhalika inaweza kuwa na faida kwao.

Ma ameahidi kuchukuwa hatua za kuwa na ushirikiano wa karibu na China ikiwa ni pamoja na mkataba wa amani kumaliza miongo kadhaa ya uhasama kati ya serikali ya China na kisiwa hicho kinachojitawala wenyewe.