1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Wito wa kutenzua mgogoro wa Zimbabwe

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYD

Mkutano wa kilele wa viongozi wa jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika,umemalizika katika mji mkuu wa Zambia,Lusaka.Mkutano huo wa SADC,umetoa mwito kwa serikali ya Zimbabwe na wapinzani wake kuwa na majadiliano kwa haraka,ili kutenzua mgogoro wa kisiasa na uchumi wa nchi hiyo.

Taarifa ya kufunga mkutano lakini haikutoa mwito kwa Rais Robert Mugabe kufanya mageuzi ya kisiasa,jambo ambalo limekosolewa na baadhi ya wajumbe katika mkutano huo.Taarifa hiyo imesifu jitahada za Rais wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki kama mpatanishi kati ya Rais Mugabe na chama kikuu cha upinzani cha Zimbabwe MDC.