1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Mke wa rais Bush ziarani Afrika

28 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnb

Mke wa rais wa Marekani bibi Laura Bush anendelea na ziara yake barani Afrika leo amezuru kituo cha matibabu ya maradhi wa Ukimwi kinacho endeshwa na kanisa mjini Lusaka Zambia.

Bibi Laura Bush amezindua kampeni ya kupambana na Malaria pamoja na mradi wa maji alipofanya ziara ya kujifahamisha mengi juu ya miradi inayopata ufadhili wa Marekani nchini Zambia.

Mapema leo bibi Bush alikutana na rais Levy Mwanawasa wa Zambia na mkewe Maureen Mwanawasa.

Hapao jana bibi Laura Bush alikuwa nchini Msumbiji ambako alitangaza msaada wa dola milioni 507 sawa na Euro milioni 377.

Akiwahutubia viongozi wa kidini na wageni mjini Maputo bibi Laura alisema.

Kuushinda ugonjwa huu kabisa ndilo hasa lengo la muhimu kwani ugonjwa wa malaria unatibika na pia unaweza kukingwa. Hapo kesho bibi Laura Bush ataelekea nchini Mali kukamilisha ziara yake katika nchi za Afrika zinazopokea ufadhili mkubwa kutoka Marekani kupambana na ugonjwa wa Ukimwi na Malaria.