1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LOS ANGELES: Waokoaji watatu wafariki

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYU

Maafisa katika jimbo la Utah nchini Marekani wanasema waokoaji watatu wamekufa na wengine sita kujeruhiwa wakati walipokuwa wakijaribu kuwafikia wachimba migodi sita waliokuwa wamekwama chini ya mgodi kwa siku 11.

Kwa mujibu wa maafisa hao tukio hilo lilitokea wakati sehemu moja ya mgodi ilipoporomoka.

Juhudi kubwa za uokozi zimekuwa zikifanywa kwenye mgodi huo tangu wachimba migodi hao sita walipofunikwa mnamo tarehe 6 mwezi Agosti.

Wanaume hao hawajafikiwa tangu ajali hiyo ilipotokea.