London:Onyo la mipango ya kigaidi Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 10.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

London:Onyo la mipango ya kigaidi Uingereza

Mkuu wa Idara ya upelelezi ya Uingereza amesema kwamba kiasi ya matukio 30 yanayohusiana na ugaidi yanapangwa nchini humo.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la upelelezi M15, Eliza Manngham Buller alisema maafisa wa upelelezi wanawasaka watuhumiwa wapatao 1,600, wengi wakiwa ni wazaliwa wa Uingereza, na wanahusishwa na kundi la Al Qaeda nchini Pakistan.

Alisema kanda za video zilizopatikana zinaonyesha kwamba wanaojitolea mhanga kwa kujiripua, ni sehemu ya watu waliokasirishwa na kile wanachokiona sera dhidi ya Uislamu, ikiwa ni pamoja na kujihusisha kwa Uingereza nchini Irak na Afghanistan.

Bibi Buller alisema Shirika la M15 limeivunja mipango mitano mikubwa ya kigaidi, tangu ilipofanyika mashambulio ya mabomu mjini London yaliowauwa watu 52.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com