LONDON:Ni miaka 10 tangu Princes Diana afariki | Habari za Ulimwengu | DW | 31.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Ni miaka 10 tangu Princes Diana afariki

Familia ya kifalme ya marehemu Princess Diana inaadhimisha kumbukumbu ya 10 tangu kifo chake kutokea ghafla mjini Paris nchini Ufaransa.Mwanawe mdogo Prince Harry aliemueleza mamake kuwa bora zaidi kote ulimwenguni na kueleza kifo chake.

''Lilikuwa tukio lililobadilisha maisha yetu milele…kama inavyotokea kwa mtu yoyote ambaye alimpoteza jamaa yake usiku huo.Cha muhimu zaidi ni kuwa tunamkumbuka kama alivyotaka kukumbukwa…kama alivyokuwa…mcheshi..aliyependa furaha..alitufurahisha sisi na watu wengine wengi.Ni imani yetu kuwa atakumbukwa hivyo na wote''

Katika hotuba yake kwenye ibada ya ukumbusho Askofu wa London Dr Richard Chatres alitoa wito wa kumalizwa kwa shaka kuhusu chanzo cha kifo chake.

Marehemu Princess Diana alipongezwa katika ibada ya ukumbusho iliyoongozwa na Askofu wa Canterbury aliye pia kiongozi wa kanisa la Kianglikana nchini Uingereza .

Diana alifariki Agosti 31 akiwa na umri wa miaka 36 pale gari aina ya Liomousine alimokuwa akisafiri pamoja na mepnzi wake Dodi al Fayed lilipopata ajali kwenye njia ya chini kwa chini mjini Paris,Ufaransa.

Ibada hiyo imefanyika katika kanisa la kijeshi karibu na Kasri la Buckingham. Hata hivyoBi Camilla aliye Duchess wa Cornwall na mkewe Prince Charles hakuhudhuria ibada hiyo kwa sababu binafsi japo alialikwa na watoto wa mume wake.Mohamed al Fayed babake mpenzi wake marehemu Princess Diana Dodi al Fayed hatahudhuria ibada hiyo kwani hakualikwa.Bwana al Fayed ni mfanyibishara mkubwa mjini London na mwenye duka la bidhaa ghali maarufu la Harrods ambako wafanyikazi wote walikaa kimya kwa dakika moja kuwakumbuka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com