1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Brown kususia mkutano iwapo Mugabe ataalikwa

Waziri Mkuu wa Uingereza Godon Brown ametishia kususia mkutano wa mwaka huu wa wakuu wa Afrika na Ulaya iwapo Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe anaalikwa.

Mkutano huo umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Ureno ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

Gordon Brown amemshutumu Rais Mugabe kwa kusababisha hali mbaya ya uchumi na maisha.

Aidha amemshutumu kwa uvunjaji wa haki za binaadamu ikiwemo matumizi ya vitisho na mateso dhidi ya upinzani.

Uchumi wa Zimbabwe kwa sasa unakabiliwa na mfumuko mkubwa kabisa wa bei huku kiwango cha wasiyo na kazi kikifikia asilimia 80.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com