1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Waziri wa Ulinzi wa Marekani yuko Uingereza

15 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaY

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates amesema kwamba Uingereza ni mshirika muhimu kabisa wa kimataifa kwa Marekani katika suala la Iraq na Afghanistan.

Gates alitowa kauli hiyo baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair na Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Des Browne mjini London kujadili mkakati mpya wa Rais George W. Bush wa Marekani kwa Iraq na mpango wa Uingereza kuondowa wanajeshi wake kutoka kusini mwa Iraq.

Ziara hiyo ya Gates inakuja ikiwa ni siku nne tu baada ya Rais Bush kusema ataongeza idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq kutoka 130,000 hadi kufikia takriban 150,000 ikiwa ni sehemu ya mkakati mpya kupambana na umwagaji damu wa kimadhehebu na mashambulizi ya waasi nchini Iraq.

Gates yuko katika ziara yake ya kwanza nchini Uingereza tokea achukuwe wadhifa huo kutoka kwa aliekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld.