LONDON: Waziri Mkuu Tony Blair atangaza mpango wa kung′atuka. | Habari za Ulimwengu | DW | 10.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Waziri Mkuu Tony Blair atangaza mpango wa kung'atuka.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, amelieleza baraza lake la mawaziri kuhusu mpango wake wa kung'atuka wadhifa wa kiongozi wa chama tawala cha Leba na pia uwaziri mkuu.

Tony Blair anatarajiwa baadaye kutangaza uamuzi wake huohadharani kwenye eneo lake la uwakilishi bungeni.

Waziri wa fedha Gordon Brown ndiye anayetarajiwa kumrithi Tony Blair.

Blair amesema ataendelea kuushikilia wadhifa wa kiongozi wa chama chake kwa kiasi miaka saba hadi pale kiongozi mpya atakapochaguliwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com