LONDON : Watuhumiwa 3 wa mashambulizi ya kigaidi mbaroni | Habari za Ulimwengu | DW | 23.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Watuhumiwa 3 wa mashambulizi ya kigaidi mbaroni

Polisi ya Uingereza imewakamata watu watatu kuhusiana na mashambulizi ya mabomu ya kujitolea muhanga maisha ya Julai saba mwaka 2005 ambayo yaliuwa wasafiri 52 katika mfumo wa usafiri wa London.

Watuhumiwa wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa Manchester ambapo walikuwa wasafiri kuelekea Pakistan. Mtuhumiwa wa tatu alikamatwa wakati akiwa nyumbani huko Leeds mji wa kaskazini ambao ulikuwa makaazi ya watu watatu waliojitolea muhanga maisha kwa kujiripuwa.

Watuhuhumiwa wamefikishwa katika kituo kikuu cha polisi mjini London kwa kuhojiwa na polisi imesema upekuzi unaendelea kwenye nyumba tano katika eneo la Leeds na katika maeneo mawili mashariki ya London.

Hadi sasa hakuna mtu eliefunguliwa mashtaka kuhusiana na mashambulizi hayo ya mwaka 2005 ambapo washambuliaji wote wanne waliojiripuwa waliuwawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com