1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London : Wanajeshi waliokamatwa wawasili kwao.

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCL

Wanajeshi 15 wa Uingereza ambao walikuwa wanashikiliwa na Iran kwa muda wa wiki mbili wamewasili nyumbano mjini London. Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini London , wanajeshi hao 15 walihamishiwa katika helikopta za kijeshi na kwenda katika kituo cha kijeshi kusini magharibi ya Uingereza ili kukutana na familia zao kabla ya kueleza yaliyowasibu.

Jana jumamosi rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad ghafla alitanzua mzuzu uliokuwa ukizidi kukua wa kidiplomasia kwa kuwapa msahama wanajeshi hao 15 ikiwa kama zawadi kwa watu wa Uingereza. Akizungumzia suala hilo kabla wanajeshi hao kuwasili mjini London, waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema huenda hivi sasa ni wakati muafaka wa kufanya mazungumzo na Iran.

Wanamaji hao walikamatwa March 23 katika eneo la maji la Shatt al-Arab kati ya Iraq na Iran. Iran inasisitiza kuwa wanajeshi hao wanamaji walikuwa katika eneo la maji la Iran, dai ambalo linapingwa vikali na Uingereza.