1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Safari kuanza tena uwanja wa Heathrow.

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgp

Shirika la ndege la Uingereza limesema kuwa lina lenga kusafirisha asilimia 95 ya wateja wake kwenda na kutoka katika uwanja wa ndege wa Heathrow kama ilivyopangwa leo Jumamosi.

Uwanja mkubwa wa ndege wa London umefunikwa na ukungu kwa siku tatu, na kusababisha misafara ya ndege kufutwa na mamia kwa maelfu ya wasafiri kukwama.

Lakini ofisi ya utabiri wa hali ya hewa nchini Uingereza inatabiri kuwa ukungu huo utaanza kuondoka, na kuyapa mashirika ya ndege siku mbili kuweza kusafirisha wasafiri ambao wamekwama waendao katika sikukuu kabla ya siku ya Chrismass hapo Jumatatu.

Wakati huo huo , ukungu mkubwa umechelewesha safari kwenda na kutoka katika mji mkuu wa India New Delhi leo Jumamosi na kuwaacha mamia kwa maelfu ya watu wakiwa wamekwama katika uwanja huo wa ndege. Lakini ukungu huo uliondoka baadaye na safari zimeanza tena.