1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Prescott asema atajiuzulu

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVQ

Naibu waziri mkuu wa zamani nchini Uingereza, John Prescott, amethibitisha leo kwamba atajiuzulu kama mbunge wakati wa uchaguzi ujao wa bunge.

Prescott mwenye umri wa miaka 69, aliwaambia wafuasi wake katika eneo analoliwakilisha bungeni la Hull Mashariki lililo kaskazini mwa Uingereza kuhusu kutaka kujiuzulu kwenye karamu iliyofanywa mwishoni mwa juma.

Katika taarifa aliyoitoa leo, John Prescott amesema imekuwa heshima kwake kuwatumikia wakaazi wa Hull Mashariki kwa miaka 37 na ataendelea kufanya hivyo hadi uchaguzi mkuu ujao nchini Uingereza.

Prescott anatarajiwa kuwajulisha rasmi wanachama wa eneo hilo kuhusu uamuzi wake kwenye mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 16 mwezi ujao.