1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Muuaji atafutwa kwa kuwauwa changudoa.

13 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjr

Msako mkubwa wa mauaji unafanyika mashariki ya Uingereza. Wapelelezi wanamtafuta mtu mmoja anayetuhumiwa kufanya mauaji mara kwa mara ambaye huwauwa watu wanaofanya biashara ya ngono.

Katika muda wa wiki moja iliyopita miili ya wanawake watano imepatikana katika eneo la Suffolk kilometa chache kutoka katika mji wa Ipswich. Wanawake hao wote walikuwa wameuwawa.