1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Mtuhumiwa wa pili atiwa mbaroni

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCi0

Mtuhumiwa wa pili ametiwa mbaroni katika uchunguzi wa mauaji ya makahaba watano katika mji wa Ipswich nchini Uingereza.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 48 anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya wanawake wote watano. Polisi bado wanamhoji mwanamume mwengine wa umri wa miaka 37 waliyemkamata mjini Felisstowe juzi Jumatatu.

Katika mkutano na waandishi habari msemaji wa polisi nchini Uingereza alisema jana kwamba mshukiwa wa kwanza ataendelea kuzuiliwa.