LONDON :Mshukiwa wa jaribio la bomu afariki | Habari za Ulimwengu | DW | 03.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON :Mshukiwa wa jaribio la bomu afariki

Mshukiwa aliyejeruhiwa vibaya na moto katika jaribio la shambulio la bomu mjini Glasgow nchini Uingereza amefariki dunia.Jaribio hilo lilitokea mwishoni mwa mwezi Juni katika kiwanja cha ndege cha Glasgow.Kafeel Ahmed mzaliwa wa Bangalore nchini India alikuwa anaendesha gari aina ya Jeep Cherokee lililogonga jingo katika sehemu ya kulaki wageni.

Mtu huyo wa umri wa miaka 27 alikuwa anapewa ulinzi mkali na polisi katika hospitali moja huko Scotland akiwa hana fahamu wakati wote huo.Ahmed alikuwa hospitali kwa takriban wiki tano baada ya asilimia 90 ya mwili wake kuchomeka vibaya sana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com