LONDON: Mshtakiwa Bilal Abdullah afikishwa mahakamani | Habari za Ulimwengu | DW | 07.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Mshtakiwa Bilal Abdullah afikishwa mahakamani

Nchini Uingereza,Muiraki alieshtakiwa kuhusika na mashambulizi ya bomu yaliyoshindwa kuripuka katika miji ya London na Glasgow amefikishwa mahakamani hii leo mjini London.Bilal Abdullah, daktari mwenye umri wa miaka 27 ameshtakiwa kula njama ya kusababisha miripuko.Daktari huyo na mwanamume mwengine,walibamiza gari lao kwenye ukuta wa jengo kuu la kupokea abiria wa ndege katika uwanja wa ndege wa Glasgow na kusababisha mripuko wa moto.Gari hilo lilipakiwa madumu ya gesi.Bilal Abdullah,aliezaliwa Uingereza na kulia nchini Irak,alizungumza mahakamani kuthibitisha tu jina lake na tarehe ya kuzaliwa.Atafikishwa tena mahakamani tarehe 27 mwezi huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com