1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Mshirika la Litvinenko haoneshi dalili ya kuugua.

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnB

Maafisa wa afya mjini London wamesema kuwa mtu wa karibu wa jasusi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko haoneshi ishara za kupatwa na sumu ya miale baada ya kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na miale hiyo ya Polonium 210.

Mshauri wa Kitaliani wa usalama Mario Scaramella alikutana na Litvinenko katika mkahawa mmoja mjini London Novemba mosi muda mfupi kabla ya kuugua na kufariki.

Scaramella alipelekwa hospitalini mjini London siku ya Ijumaa baada ya miale kugundulika mwilini mwake.

Mjane wa Litvinenko pia amepatikana na miale hiyo. Maafisa wa Uingereza wanachunguza watu 24 na kupekua maeneo kadha yanayohusiana na tukio hilo.