LONDON : Mpango wa uhuru wa Kosovo ungalipo mezani | Habari za Ulimwengu | DW | 10.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Mpango wa uhuru wa Kosovo ungalipo mezani

Mwanadiplomasia wa Ujerumani Wolfgang Ischinger amesema mpango wa Umoja wa Mataifa kuipa uhuru Kosovo kutoka Serbia bado uko mezani.

Ischinger ambaye amechaguliwa kuwa mjumbe wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo ya hivi karibuni kabisa juu ya hatima ya ya mustakbali wa Kosovo alikuwa akizungumza mjini London baada ya mkutano wa awali na wajumbe wenzake wa Marekani na Urusi. Wajumbe hao wanatarajiwa kwenda Belgrade na Pristina mwishoni mwa juma kwa kile Umoja wa Ulaya na Marekani wanachotumai kuwa itakuwa ni duru ya nwisho ya mazungumzo juu ya jimbo hilo linalokaliwa na watu wengi wa kabila la Waalbania.

Urusi ambaye ni mshirika wa Serbia hadi sasa imezuwiya kupitishwa kwa mpango huo wa Umoja wa Mataifa katika Baraza la Usalama.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com