1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Mjane wa Litvinenko azungumza kwa mara ya kwanza

10 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCke

Mjane wa mpelelezi wa zamani wa Urusi aliyeuwawa kwa kupewa sumu Alexander Litvinenko anaamini kwamba maafisa wa serikali ya Urusi yumkini wakawa wamehusika na kifo cha mume wake.

Kwa mujibu wa mahojiano na gazeti la Uingereza la Mail litolewalo kila Jumapili Marina Litvinenko ingawa hakumuelekezea kidole cha shutuma moja kwa moja Rais Vladimir Putin wa Urusi amedokeza kwamba kutokana na hali ya kisiasa iliopo hivi sasa nchini Urusi inafanya kitendo hicho kiwezekane.

Marina Litvinenko amesema anaamini kwamba wapelelezi wa Uingereza watawatambuwa wauuaji wa mume wake na kuongeza kusema wamba hana imani na wapelelezi wa Urusi kwa kuwa haamini kuwa wataeleza ukweli.

Mjane huyo pia amesema kwamba maisha nchini Uingereza yaliwadanganya kwa kuhisi kuwa wako salama.