LONDON ; Meli yaponea chupu chupu kugonga jukwaa la gesi
12 Januari 2007Matangazo
Meli ya mizigo katika Bahari iliochafuka ya kaskazini imeponea chupu chupu kugongana na majukwa mawili ya gesi baharini na tishio hilo lililazimisha wafanyakazi watelekeze mojawapo ya majukwaa hayo na kusitisha uzalishaji.
Tishali moja liko njiani kwenda kuivuta meli hiyo ufukweni inayoitwa Vindo na wafanyakazi wake tisa
Awali ilielezwa kwamba meli hiyo ya tani 3,000 iliopoteza nguvu za engine yake ilikuwa igongane na jukwaa hilo la gesi wakati ikielea kati ya Scotland na Norway.
Hali ya tahadhari ilitangazwa hapo jana usiku baada ya meli hiyo ilioandikishwa Antigua na Bermuda ikiwa na shehena ya tani 4,200 za mbolea ilipokuwa ikielea karibu na majukwaa hayo ya kuchimba gesi baharini.