LONDON: Matamshi ya Dannat yanaakisi mkakati wa Blair | Habari za Ulimwengu | DW | 14.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Matamshi ya Dannat yanaakisi mkakati wa Blair

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema matamshi ya mkuu wa majeshi ya Kingereza,Jemedari Richard Dannatt yanaakisi mkakati wa serikali yake.Jemadari Dannat juma hili alishauri kuwa vikosi vya Kingereza virejeshwe nyumbani kwa haraka kutoka Irak.Blair alipozungumza na maripota huko Scotland alisema anahisi kuwa katika mahojiano ya Dannat yaliyochapishwa gazetini siku ya Ijumaa,baadhi ya matamshi yake yamechukuliwa visivyo.Katika mahojiano hayo Jemadari Dannatt alinukuliwa kusema kuwa vikosi vya Kingereza nchini Irak vinasababisha hali ya mambo kuwa mbaya zaidi katika nchi hiyo.Hivi sasa Uingereza ina kama wanajeshi 7,000 nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com